Posts

Ramos ashangazwa na uwezo wa Bale lakini anasema hawakutayarishwa juu ya ujio wake.

Image
Gareth Bale akiwasili Istanbul akiwa na Real Madrid kuwakabili Galatasaray. Galacticos Cristiano Ronaldo amesaini mkataba mwingine wa miaka mitano...

Kaka aambia Milan kutomlipa mshahara

Image
Kaka Mchezaji wa kiungo cha kati wa AC Milan Kaka ameitaka kilabu yake kutomlipa mshahara wake huku akiendelea kupona kutokana na jereha lake la paja ambalo alilipata wakati wa mchezoo wake wa kwanza tangu kujiunga na kilabu hiyo. Mchezaji huyo wa kimataifa wa timu ya Brazil aliondolewa uwanjani na jeraha hilo katika dakika ya 70 ya mechi waliyokwenda sare ya mabao mawili na timu ya Rossoneri.

Mdhalilishaji aliyejidai kuwa Justin Bieber

Image
  Rober Hunter aliwahidi watoto kuwa angekuwa na uhusiano wa kimapenzi nao Mwanamume mmoja nchini katika kitongoji cha Middlesbrough, Uingereza aliyejidai kuwa mwanamuziki maarufu duniani , Justin Bieber, ili kuwahadaa watoto kuweza kumtumia kanda za video wakiwa wanafanya vitendo vya ngono, amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela. Robert Hunter, mwenye umri wa miaka 35, na ambaye alijidai kuwa 'Justin Bieber Hunter 'alikamatwa baada ya msichana mmoja kutoka Tasmania kufahamisha polisi kumhusu

RONALDO KUSALIA BERNABERU HADI 2018

Image
Ronaldo anasema Man U ni mambo ya zamani Cristiano Ronaldo amesema kuwa anataka kusalia kuwa Real Madrid kama mchezaji soka baada ya kutia saini mkataba mpya na mabingwa wa ligi ya Uhispania hadi mwaka 2018. Ronaldo ambaye ni mchezaji muhimu wa timu yake ya taifa ya Ureno, awali ilisemekana alikuwa anaelekea Machester United kilabu yake ya zamani....

Ghana kukutana na Misri kutafuta nafasi Brazil

Image
Mashabiki wa soka Ghana wanatumai kuwa nchi yao itafuzu Brazil 2014 Ghana itamenyana na Misri katika mechi za kuamua nchi ya Afrika itakayowakilisha bara zima katika dimba la kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil. Misri kama nchi pakee ambayo imeshinda mechi zake zote za makundi za kufuzu kushiriki kombe la dunia, bila shaka imeitia hofu nchi zengine na bila shaka hakuna ambaye angependa kukukutana nao. Taarifa zinazohusiana...

KESI YA WAZIRI MKUU PINDA YAANZA KUSIKILIZWA SERIKALI YATOA PINGAMIZI KALI

Image
Kesi inayomkabili waziri mkuu Mizengo  Pinda na mwanasheria mkuu wa serikali  imetajwa mahakamnai kwa mara ya  kwanza ambapo  wamewasilisha pingamizi  la  awali dhidi ya  kesi ya kikatiba waliyofunguliwa na kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu  kwa kushirikiana na chama cha wanasheria Tanganyika.    Katika kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013, LHRC na TLS,wanadai kuwa Pinda alivunja katiba kutokana na kauli  aliyoitoa bungeni hivi karibuni  wakidai kuwa ni amri kwa vyombo vya utekelezaji wa sheria kuwapiga wananchi  wakati wa vurugu.    Hata hivyo Pinda na  mwanasheria mkuu  kwa pamoja katika majibu yao ya madai hayo, wamewasilisha pingamizi la awali ambapo  pamoja na mambo mengine wamedai   kuwa walalamikaji na watu  walioorosheshwa katika kesi hiyo hawana mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo.

YANGA YAKAZIWA NA MBEYA CITY , YALAZIMISHA SARE YA 1-1, MNYAMA ATAFUNA MIWA YA MTIBWA TAIFA, AZAM WAPONEA CHUPUCHUPU KAITABA, JKT RUVU WAZIDI KUPAA KILELENI!!

Image
MZUNGUKO wa tatu wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 umeendelea kushika kasi leo hii kwa timu zote 14 kushuka katika viwanja saba tofauti nchini. Mabingwa watetezi, klabu ya Yanga ya Dar es salaam wameponea chupuchupu mbele ya Wenyeji wa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, klabu ya Mbeya  City ambapo wamelazimishwa  sare ya 1-1, huku wakishuhudiwa na mwenyekiti wake Yusuf Manji aliyewasili leo mchana. Mbeya City wanaofundishwa na Juma Mwambusi ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 49 kupitia kwa Mwagane Yeyah na Yanga walisawazisha bao hilo katika dakika ya 71 kupitia kwa Mrundi, Didier Kavumbagu “Kavu”. Mbeya City walianza kwa kasi mchezo huo huku wakionana kwa pasi safi na kushambulia lango la Yanga kama Nyuki, lakini makosa ya washambuliaji yaliwanyima mabao ya wazi.   Hata hivyo kipindi cha pili Yanga walianza kwa kasi na kushambulia lango la wapinzania wao, lakini dakika za lala salama wakakoshwa bao...