MWAKA UNAISHA, ANZA UPYA KWA MWENZI WAKO!
HUU ni msimu wa sikukuu! Juzi, tumesherehekea Sikukuu ya Krismasi na sasa tunaelekea Mwaka Mpya 2014. Kwa nguvu za Mungu tutafika salama. Ndugu zangu, hebu tutafakari vizuri kuhusu mwaka uliopita na kuangalia cha maana tulichofanya kwa wenzi wetu.