Libya washinda CHAN 2014
Libya mabingwa wa CHAN 2014 Libya imepata ushindi wake wa kwanza wa kombe la taifa bingwa Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Ghana mjini Cape Town Afrika Kusini. Mechi ya fainali kati ya nchi hizo mbili ilikamilika kwa sare tasa kabla ya Joshua Tijani wa Ghana kukosa bao la penalti na kuipa Libya ushindi wake.