POLISI SASA NI KONDA
SOMA UTAJIFUNZA KITU KIKUBWA SANAA,. MAISHA ni mapambano. Kuna kupanda na kushuka na Waswahili wana usemi unaosema ‘Kesho yako anaijua Mungu’. Usemi huu unathibitishwa na Farahana Mwanjonde (40), ambaye alikuwa askari polisi na sasa ni utingo wa daladala. Nilivutiwa na muonekano wake na uchangamfu wake, hasa pale anapopishana na trafiki barabarani, ambapo huwa wanamchangamkia. Siku niliyomhoji Farahana alinieleza kuwa aliwahi kuwa polisi na kwamba anapitia changamoto nyingi katika maisha. Lakini, ukimuangalia tabasamu lake,