Zitto ataja vigogo walioficha fedha nje
WAKATI ripoti ya kamati iliyoundwa na serikali kuchunguza tuhuma za vigogo walioficha fedha kwenye mabenki ya nje ya nchi ikiwa bado haijatolewa bungeni, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amewataja vigogo watatu kuwa miongoni mwa wahusika. Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Bara), ndiye muasisi wa hoja hiyo bungeni. Hivi karibuni alitishia kuwataja wahusika endapo serikali haitawasilisha ripoti hiyo kwenye mkutano wa Bunge uliomalizika Jumamosi. Mbunge huyo aliwataja vigogo hao juzi wilayani Kaliua mkoani Tabora wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Kolimba. Bila kutaja majina yao, Zitto aliwataja kwa nyadhifa zao walizowahi kushika akisema ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ulinzi wa zamani na aliyewahi kuwa m