JINSI FIESTA 2013 ILIVYOKUWA JIJINI MBEYA SOKOINE WALIVYO JITOKEZA
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga za muziki huo,Neylee akiimba kwa hisi jukwaani huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kwa shangwe ndani ya uwanja wa Sokonine. Wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine,ndio kwanza shoo inaanza ambapo msanii aliyewahi kuiwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu. Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea usiku huu kwenye uwanja wa Sokoine,Mkoani Mbeya Mama wa miduara ya Kibongofleva,Shilole akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya. Sehemu ya umati wa watu. Mkali mwingine wa hip hop (bongofleva),Ney wa Mitego akikamua jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013,kwenye uwanja wa Sokoine,mjini Mbe...