Posts
Showing posts from November 25, 2013
900 waliuawa katika vita dhidi ya M23
- Get link
- X
- Other Apps
Wanajeshi wa DRC Jeshi la congo linasema kuwa mapigano na waasi wa M23 yamesababisha vifo vya zaidi ya wapiganaji 900 tangu mwezi Mei. Msemaji wa jeshi Genarali Jean-lucien Bahuma alisema kuwa takriban wanajeshi 200 na zaidi ya wapiganaji 700 waliuawa katika mapigano katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Wanajeshi watatu wa amani wa UN pia waliuawa kwenye makabiliano hayo.
TAARIFA YA ZITTO ZUBERI KABWE (MB) KUHUSU KUVULIWA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA CHA CHADEMA
- Get link
- X
- Other Apps
1. Utangulizi Katika kikao chake cha siku mbili kilichofanyika tarehe 20 - 22 Novemba 2013, Kamati Kuu ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama. Kwa mujibu wa taarifa ya chama iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za kuvuliwa uongozi mimi na Dk Kitila Mkumbo ni uhaini na hujuma kwa chama kutokana na waraka unaojulikana kama mkakati wa uchaguzi 2013. Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika Kikao cha Kamati Kuu.
ADEN RAGE ATISHIWA KUUAWA NA SIMBA
- Get link
- X
- Other Apps
Ismail Aden Rage. MWENYEKITI aliyesimamishwa Simba, Ismail Aden Rage, ameanza kupata wakati mgumu baada ya kutishiwa kuuawa endapo ataendelea kung’ang’ania madarakani. Rage amethibitisha kuhusiana na hilo jana wakati akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kamati ya utendaji ya klabu hiyo, kutangaza kumsimamisha katika nafasi hiyo, katika kikao chao kilichofanyika mapema wiki iliyopita jijini Dar ambapo tukio la kushangaza ni kitendo cha mwenyekiti huyo kukataa maswali yoyote kutoka kwa