Posts

Showing posts from August 27, 2013

Mashairi Ya Wimbo Mpya Wa Young Killer - Mrs Super Star Yako Hapa.

Mashairi Ya Young Killer - Mrs Super Star Kila mwanadamu anaupendo. mwingne anawaza., vp atampataje,amtakaye.. sio kwamba na act..no niko real... japo msodoki ni mdogo.,ila nauwezo waku feal... fikra zangu zinani2ma nidate kwa maunda zoro. najua ntaleta jiras kwa brother.,banana zoro Lyrics Exclusive On Sammisago.com xaxa vp ningekua na penny,.iv ntakua free... au kama ni ngekua na mwasit wa t.h.t.. ila penny na his diamond atanisumbua., hata mwasiti najua pendo  langu ata livua... Lyrics Exclusive On Sammisago.com kwanza long time agoo., nishazimikaga na wema ila skendo za magazet daaa.. moyo wangu ukamtema,... nikachukia mapapalazi niakahis wameharibu bahat.. moyo wangu nikauweka bondi..kwa chiku mwanaharakati... ila wote 2nachana hatuta dumu magetoni,.. nklipozimika na besta..marlow akapiga honi,.. madam Lita na salama nikaogopa mcharuko wa b.s.s.... nimemove mpaka dar wolper ni mchane face 2 face.... ila roho inakata...

Zitto: Sitogombea Urais wala Ubunge 2015

Image
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015. Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili. Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015. Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA). "Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na siasa kwani nimechoka...

EAC YAINGILIA KATI MZOZO WA TANZANIA NA RWANDA

Image
Wakati Tanzania ikisema kuwa iko tayari kukaa meza moja na jirani yake Rwanda kumaliza hali ya uhasama iliyoanza kujitokeza katika siku za hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Richard Sezibera amesema jitihada za kidipolomasia zinafanyika kutatua tofauti hizo za kimawazo.    Bila kutaja taasisi wala wanaohusika katika jitihada hizo za kidiplomasia, Dk Sezibera aliwaambia waandishi wa habari jijini Arusha jana kuwa jitihada hizo zinafanyika kimya kimya bila kushirikisha vyombo vya habari “Migongano na tofauti za kimtazamo miongoni mwa viongozi wakuu wa nchi wanachama wa EAC ni jambo lisilo la afya kwa Jumuiya na linastahili kushughulikiwa kidiplomasia,” alisema Dk Sezibera.   Akizungumza kwa tahadhari kubwa kukwepa kuingia kwa undani kuhusu suala hilo, Katibu Mkuu huyo alisema inafaa kila linalowezekana lifanyike kutatua mgongano wowote unaotokea kati ya viongozi wakuu. ...