Mshambuliaji wa kujitolea mhanga amejiripua kwenye mkahawa uliojaa watu katika mji wa Beledweyne, katikati mwa Somalia. Watu kama 16 wameuwawa na zaidi ya 30 kujeruhiwa. Kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabab, limesema limefanya shambulio hilo. Serikali ya Somalia, ikisaidiwa na kikosi cha wanajeshi kutoka nchi kadha za Afrika, inapigana na Al Shabab ili kuidhibiti nchi.