USAJILI WA ANDER HERRERA KWENDA MAN UNITED UMESHINDIKANA KUTOKANA NA SHERIA YA KODI NCHINI HISPANIA
Usajili wa kiungo wa kihispania Ander Herrera umeshindikana baada ya ucheleweshwaji wa mambo na taratibu za usajili kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Japokuwa inasemekana kwamba United walikubali kulipa kiasi cha €36 million ili kumsajili kiungo huyo , vyanzo mbalimbali kutoka nchini Spain vi nasema kwamba masuala kadhaa ya sheria ya kodi nchini Hispania yalisababisha dili hilo lisifanyike. Mtandao wa ESPN unaripoti kwamba kutoka na masuala ya kodi gharama nyingine zisi zo zidi kiasi cha €6m zilisababisha United kushindwa kuk amilisha usajili wa mchezaji huyo ambaye amekuwa kwenye kiwango bora sana katika timu ya Bil bao . United tayari walishamtaarishia namba ya jezi na maslahi binafsi yalishafanyika , huku Herrera akikub ali kukubali kupunguzwa kwa maslahi yake binafsi ili kukamilisha usajili huo. Lakini pamoja na kushind ikana kwa dili katika dirisha hili, inaaminika United watarudi tena kwa kiungo huyo katika dirisha la usajili la mwezi Janu...