Mwandishi:Samwel mlawa Kuna usemi flani unatumiwa na watu wengi sana. unasema; “kazi ndio msingi wa maendeleo ya mtu yeyote” . Hata mimi nakubaliana na usemi huu kwani ni kweli kabisa kazi ndio msingi wa hatua yoyote ya maendeleo ya mtu yeyote chini ya msingi mkuu ambao ni Mungu. Kinyume chake, asiyefanya kazi (ya kuajiriwa/kujiajiri) basi atabaki kuwa maskini na mtu wa shida ya kipato, mahusiano mabaya na wanadamu wenzako, kuwa tegemezi nk. Kwa kuwa tunatamani sana kutoka katika kongwa hili la umasikini wa kipato na hali mbaya ya maisha, tunalazimika kufanya jukumu letu kuu la kumuomba sana Mungu ili atuwezeshe kujua na kufahamu mbinu mbalimbali kisha kujifunza na kufahamu kwa makini tena kwa njia rahisi mno za kututoa katika hali hii ya umaskini uliokithiri. Ikumbukwe kwamba, kujifunza kwa msisimko tu bila ya kuyaingiza mambo hayo uliyojifunza katika mazoezi na vitendo vya makusudi maishani mwetu ni wazi kwamba hayatatusaidia, bali yatabaki vichwani mwetu...