JITAMBUE:UHUSIANO KATI YA MAPENZI NA HOFU.
SAYANSI ya mapenzi inakataa kuwepo mapenzi ya kweli sambamba na hofu. Mtu hawezi kusema anampenda mwenzake wakati kuna vitu anaviogopa kutoka kwa mpenzi wake kiasi cha kumuondolea ujasiri. Ifahamike kwamba, ukamilifu wa mapenzi kwa ni namna hofu inavyoweza kushughulikiwa na kuondoshwa kabisa miongoni mwa wapendanao. Uchunguzi unaonyesha kwamba, woga umekuwa sumu kubwa ya mapenzi na mara nyingi imebainika kwamba, kila woga unavyozidi kumwingia mtu ndivyo anavyopoteza mshawasha wa kupenda. Tunafahamu ubora wa majiko ya gesi lakini wengi wamekuwa hawataki kuyatumia kwa sababu wanaogopa kulipukiwa, hivyo kuamua bora watumie kuni, mkaa au mafuta ya taa ambayo wanaamini ni salama. Hii ina maana kwamba, mwanamke au mwanaume anaweza kuwa tayari...