Posts

Showing posts from November 22, 2013

Walcott kurudi uwanjani?

Image
                          Walcot amekuwa akiigua kwa kwaribu miezi miwili Theo Walcott huenda akaichezea Arsenal siku ya jumaamosi ikiwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miezi miwili baada ya kupona kutokana na majeruhi ya tumbo. Walcott yumo katika kikosi cha kupambana na klabu yake ya zamani Southampton siku ya Jumaamosi.

WARAKA ULIOWAVUA VYEO ZITTO, DK KITILA NA MWIGAMBA HUU HAPA

Image
  Zitto Kabwe. MKAKATI WA MABADILIKO 2013 UTANGULIZI: Taasisi tunayoizungumzia ilisajiliwa rasmi mwezi January 1993 na tokea wakati huo imeongozwa na wakuu wa taasisi wapatao wawili na aliyepo kwa sasa ni wa tatu. Wa kwanza aliongoza kwa miaka mitano tangu wakati huo 1993 hadi 1998 na kumwachia aliyefuata ambaye naye aliongoza kwa miaka mitano hadi mwanzoni mwa 2004 na kumwachia aliyepo sasa. Huyu aliyepo aliongoza kwa miaka mitano tangu mwaka 2004 hadi 2009 na kisha akachaguliwa tena mwaka 2009 kwa kipindi cha pili. Tunapenda kwa hatua ya mwanzo kabisa kutambua juhudi za wakuu wetu wote waliopita walizozifanya katika kuhakikisha taasisi yetu inakua kwa kutumia uwezo wote waliokuwa nao na katika mazingira yaliyowakabili. Mwaka 1995 chini ya mkuu wa kwanza tulipata wawakilishi watatu kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi. Mwaka 2000 chini ya mkuu wa pili tukapata wawakilishi wanne pamoja na wa nyongeza mmoja na kufanya idadi kuwa watano. Mwaka 2005 chini ya mkuu

Rage arudishwa madarakani

Image
Ismail Aden Rage. BARAZA la Wadhamini la Klabu ya Simba, limesikia maamuzi yaliyofanywa na kikao cha kamati ya utendaji ya timu hiyo, juu ya kumsimamisha mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage na kusema lenyewe bado linamtambua kiongozi huyo.

RONALDO: NATAKA KUMALIZIA SOKA LANGU BERNABEU - SINA UHAKIKA KAMA NITAHUDHURIA SHEREHE ZA BALLON d'OR"

Image
                   Cristiano Ronaldo   amesisitiza kwamba hana nia ya kuondoka Real Madrid , akikiri kwamba anafikiria kumaliza maisha yake ya soka ndani ya Santiago Bernabeu. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 ambaye alihusishwa sana na kurudi Manchester United mapema mwaka huu, baada ya kusema kwamba hana furaha ndani ya mji mkuu wa Spain, lakini mwishowe akaamua kusaini mkataba mpya utakaomfanya abaki na  Los Blancos mpaka June 2018.

CHADEMA CHAMSIMAMISHA UONGOZI ZITTO NA DR MKUMBO

Image
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba wamevuliwa vyeo vyao vyote baada ya kuhusika na waraka wa mkakati wa siri wa kukipasua chama unaojulikana kama 'Waraka wa Ushindi' ambao umevunja katiba za chama hicho, kupandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa chama. Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Mhe. Tundu Lissu akieleza maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema kwa wanahabari (hawapo pichani). SABABU ZA ZITTO, DK. KITILA NA MWIGAMBA KUVULIWA VYEO VYAO Mhe. Tundu Lissu amesema kuwa Kamati Kuu imenasa waraka huo wa mkakati wa siri wa kukipasua chama vipande vipande unaohusisha watu wanne ambao ni Zitto Kabwe, Dk. Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana.