Posts

Showing posts from October 21, 2013

Passion love poem........ Everyone needs love to live!!!!

Image
Body can explain, Things amazingly. Stay a little closer to me, Hold me and kiss me tenderly, It may feel sparkling your inside, There may not any words to explain it, But never feel fear, Coz' not only words, But also Body can explain, Things amazingly.

Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu yabariki Saudi Arabia kukataa uanachama katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

Image
Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Saud al-Faisal katika moja ya mkutano Reuters/路透社 Jumuiya ya nchi za kiarabu imeunga mkono hatua ya Saudi Arabia kutupilia mbali nafasi ya uanachama wa muda iliyopewa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa madai kuwa baraza hilo limeshindwa kusuluhisha mizozo katika nchi za kiarabu.

Dakar kumzika Kocha wa zamani Bruno Metsu

Image
Bruno Metsu kuagwa na kuzikwa nchini Senegal Raia nchini Senegali mjini Dakar wanatarajia kuhudhuria mazishi ya Kocha Mfaransa Bruno Metsu ambaye aliaga dunia juma lililopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani . Mfaransa huyo ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 59 alichangia sana kuifikisha timu ya Senegali hatua ya robo fainali ya michuano ya kuwania kombe la dunia 2002 michuano iliyofanyika nchini Japan. Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka barani ulaya kupitia mtandao wake,kocha huyo amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani na mauti yalimfika akiwa Ufaransa

DRC yasitisha mazungumzo na M23

Image
Waasi wa M23 wanaolalamikiwa kuvuruga amani ya Mashariki ya Kongo Mazungumzo ya amani kati ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 yamesitishwa tena licha ya Umoja wa Mataifa kuweka msukumo wa kuendelea kwa majadiliano ya pande hizo mbili. Mazungumzo hayo yamekuwa yakiendelea mjini Kampala Uganda tangu Septemba mwaka huu ambapo kila upande umetoa tamko lake kuhusiana na kusitishwa kwa mazungumzo hayo

YANGA WATANGULIA LAKINI JE WALIFIKA?

Image
Baadhi ya mashabiki walizima kwa mshangao wa kilichokuwa kinaendelea uwanjani Ama kweli kutangulia si kufika,au kama wanavyosema wakongomani kuwa KOKENDE LIBOSO,EZA KOKOMATE. Usemi huo ulidhihirika hapo jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya Mabingwa watetezi Ligi kuu soka Tanzania Bara Timu ya Yanga,pamoja na kutangulia kufunga bao 3 dhidi ya Simba hadi mapumziko,walijikuta wakiambulia sare ya bao 3-3 hadi Mwisho wa mchezo baada ya Simba kusawazisha bao zote katika Kipindi cha Pili.