MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT JIJINI MBEYA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 NA VIBOKO 12 BAADA YA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI
MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT JIJINI MBEYA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 NA VIBOKO 12 BAADA YA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19. Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemtia hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19). Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji. Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa...