Posts

Showing posts from July 31, 2013

Fahamu mambo mengi kuhusiana na Ndizi kuwa sehemu ya maisha yako.

Image
Ndizi ni tunda ambalo limezoeleka kwa watu wengi , linapatikana karibu kila mahali . Hata hivyo inawezekana ukawa hujafahamu umuhimu wa tunda hili mwilini mwako . Taarif aifuatayo itabadilisha mtazamo wako kwa tunda hili na utafahamu kwanini hupaswi kulichukulia poa hata siku moja . Ndizi mbivu zina sukari zinazohitajika kwenye mwili wako , sukari hizi ni zile ambazo zinafahamika kwa majina ya kitaalamu ya Sucrose , Fructose na Glucose ambazo kwa pamoja zimechanganyikana na Fibre muhimu ambazo zinalifanya tunda hili kuwa chanzo muhimu cha nishati au nguvu inayohitajika mwilini mwako . Utafiti umeonyesha kuwa ndizi mbivu mbili zinatosha kukupa nishati ambayo utaitumia kwa mazoezi ya nguvu ya dakika 90 ambazo ni sawa na saa moja na nusu . Hii ndio sababu wanamichezo wengi hutumia ndizi mbivu kabla na baada ya mazoezi mazito na wakati mwingine kabla na baada ya mashindano katika mchezo husika . Nishati si faida pekee inayokuja kwenye tunda la ndizi , tunda hili lin...

Jipya lililosemwa na Serikali kuhusu kodi ya simcard Tanzania

Image
Ni kuhusu kauli ya serikali kuhusu ile ishu iliyochukua sana headlines ya kodi ya simcard Tanzania ambapo kwenye Exclusive na Gazeti la Nipashe, Waziri wa fedha katoa ya moyoni. Anakwambia Serikali imekubali kwamba kodi mpya ya laini ya simu ni mgogoro na inakusudia kurejesha muswada wa sheria ulioanzisha kodi hiyo bungeni kwa mjadala zaidi kuanzia mwishoni mwa mwezi ujao. Kingine alichosema ni hiki… ‘hili swala kwa sasa linashughulikiwa kwa mapana zaidi na Serikali na linatarajiwa kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi, Wabunge watapata nafasi ya kulijadili na muafaka utapatikana’  wakati hiyo kauli ikitoka kwa Waziri wa fedha, leo utaratibu wa makato ya laini ya simu kwa shilingi elfu moja unatarajiwa kuanza kwa kampuni zote za simu Tanzania

KAULI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ITAMFIKISHA KORTINI"WAPIGWE TU"

Image
KAULI ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ya kubariki vyombo vya dola kuendeleza kipigo kwa raia wanaokaidi amri imechukua sura mpya baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu (LHRC) kutangaza kumburuza mahakamani wiki hii kutokana na kushindwa kufuta kauli yake. Juni 20, mwaka huu, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni, Waziri Mkuu, Pinda, alivitaka vyombo vya dola kuendelea kuwapiga raia, akisema kuwa hakuna namna nyingine kwani serikali imechoka. Kauli hiyo imekuwa ikipingwa na wananchi, mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanasiasa wakimtaka Waziri Mkuu, Pinda, kuifuta kwa kuomba radhi, wakidai kuwa inachochea uvunjifu wa sheria. Akitangaza kusudio la kituo hicho kufungua kesi dhidi ya Pinda, Mkurugenzi wa maboresho na utetezi, Harold Sungusia, alisema hadi jana walikuwa tayari wameandaa kusudio la shtaka lao. Alisema kuwa kisheria kilichowafanya kufikia uamuzi huo ni kutokana na waziri mkuu huyo kukiuka Katiba ya nchi inayozungumzia u...