VITA YA WATANI WA JADI J'PILI
KESHOKUTWA Jumapili litapatikana jibu la nani mbabe katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara ambayo itawakutanisha watani wa jadi, msimu huu. Simba watakuwa wenyeji wa Yanga, kila upande utakuwa unacheza mechi yake ya tisa ya ligi hiyo msimu huu, huku mabingwa watetezi wakionekana kupania kupanda na Simba kutaka kujichimbia zaidi kileleni. Simba ina pointi 18 kileleni wakati Yanga ina 15 katika nafasi ya nne, iwapo Simba itateleza basi zitalingana pointi. Takwimu zinaonyesha Simba inafanya vizuri zaidi hadi sasa lakini zile za uzoefu wa mechi za watani, Yanga wanaonekana kuwa na kikosi imara zaidi. Inaonyesha lazima ‘mtu atakaa’, lakini si rahisi kung’amua ni yupi.