Posts

Showing posts from September 9, 2013

WAZIRI MAGUFULI AZOMEWA MBELE YA RAIS

Image
RAIS Jakaya Kikwete jana alipata wakati mgumu, baada ya kukutana na nguvu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mwanza katika ziara yake, huku Waziri wake wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, naye akijikuta akizomewa mbele yake. Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA. Hata hivyo maofisa usalama walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara. Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika. Baada ya viongozi wote kutambulishwa bila Wenje kutajwa, wananchi walianza ...