Posts

Showing posts from August 14, 2017

NAMNA YA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI

A.KWA NINI KUKU WA KIENYEJI? 1. Wastahimilivu wa magonjwa lakini ni muhimu wakikingwa na magonjwa ya kuku kama mdonde, ndui ya kuku n.k ili kuweza kuwaendeleza. 2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini. 3. Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa na kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu kama ukame, baridi n.k 4.Nyama na mayai yake vina ladha nzuri