MPENZI WAKO NDIYE ADUI WAKO...
MPENZI WAKO NDIYE ADUI YAKO IMEANDIKWA NA MLAWA,S.S MAPENZI Kila binadamu hupenda jambo fulani. Mapenzi ya mtu juu ya jambo yaweza kumvutia kiasi kwamba anaweza kupoteza welekeo wa maisha yake. Watu hupenda hadi kileleni. Hapa ndipo mtu aelewi hili wala lile. Hali hii si tu kwa vijana wanaoingia katika umri wa balehe bali hata kwa wale waliovuka umri huu. Kweli kila mtu anahaki ya kupenda. Na mapenzi haya yalianza pale binadamu walipoanza kuishi pamoja kama mke na mume kama vitabu vyetu vya dini vinavyoelekeza, ambavyo ni Biblia na Kuruhani.