"LEO NITAWAANIKA VIGOGO WOTE AMBAO NI WAUZA UNGA ".....MWAKYEMBE
Siku moja baada ya kufanya ziara ya ghafla Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema leo ataweka hadharani majina ya watu wanaosafirisha dawa za kulevya nchini. Dk Mwakyembe juzi alifanya ziara hiyo JNIA kukagua utendaji kazi kwenye uwanja huo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea kashfa ya kupitishwa kwa dawa za kulevya na baadhi ya Watanzania wakiwamo wasanii kukamatwa sehemu mbalimbali duniani. Aidha, hatua ya waziri huyo imekuja siku tatu baada ya ahadi aliyotoa akiwa Mwanza kwamba katika kipindi cha wiki mbili kuanzia juzi, atahakikisha anawakamata vigogo wote walio katika mtandao wa usafirishaji na uingizaji wa dawa za kulevya kupitia viwanja vyote vya ndege nchini. Akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vijana iliyoandaliwa na Taasisi ya Jitambue Foundation, yaliyofanyika k...