KESI YA WAZIRI MKUU PINDA YAANZA KUSIKILIZWA SERIKALI YATOA PINGAMIZI KALI
Kesi inayomkabili waziri mkuu Mizengo Pinda na mwanasheria mkuu wa serikali imetajwa mahakamnai kwa mara ya kwanza ambapo wamewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya kikatiba waliyofunguliwa na kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu kwa kushirikiana na chama cha wanasheria Tanganyika.
Katika
kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013, LHRC na TLS,wanadai kuwa Pinda
alivunja katiba kutokana na kauli aliyoitoa bungeni hivi karibuni
wakidai kuwa ni amri kwa vyombo vya utekelezaji wa sheria kuwapiga
wananchi wakati wa vurugu.
Hata
hivyo Pinda na mwanasheria mkuu kwa pamoja katika majibu yao ya madai
hayo, wamewasilisha pingamizi la awali ambapo pamoja na mambo mengine
wamedai kuwa walalamikaji na watu walioorosheshwa katika kesi hiyo
hawana mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo.
Kesi
hiyo inasikilizwa na jopo la majaji watatu likiongozwa na jaji
kiongozi, Fakihi Jundu akisaidiana na jaji Dk Fauz Twaib na jaji
Augustine Mwarija ambapo upande wa wadaiwa uliwakilishwa na mawakili wa
serikali wakuu watatu, Nickson Mtingwa, Sarah Mlipana na Alesia Mbuya.
Aidha
upande wa walalamikaji uliwakilishwa na mawakili wanne kati ya saba
waliotajwa awali .Akizungumza na waandishi wa habari nje ya
mahakama hiyo, mmoja ya mawakili hao amesema wamepewa siku 14 kujibu
pingamizi lililotolewa .
Wakati
kesi hiyo ilipotajwa mahamani hapo upande wa madai uliomba siku 21
kuwasilisha majibu ya wadaiwa ambapo hata hivyo wakili wa
serikali mkuu, Mtingwa, alipinga ombi hilo katika kipengele cha muda
ulioombwa na badala yake akapendekeza wapewe siku 14 tu.
Mahakama
katika uamuzi wake uliosomwa na jaji kiongozi Jundu, ilikataa ombi la
wadai na kukubaliana na ombi la wadaiwa, na kuwapa wadai siku 14 badala
ya siku 21 kama walalamikaji walivyomba ili kuweza kuwasilisha majibu
yao.
Mahakama
hiyo iliamuru wadai wawasilishe mahakamani majibu yao kabla au
septemba 30, na kupanga kusikiliza pingamizi la awali la wadaiwa oktoba
18.
Comments
Post a Comment