REGINALD MENGI NA WAZIRI SOSPETER MUHONGO WASHIKANA MASHATI
MWENYEKITI Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wameingia katika mzozo mzito kuhusu uwekezaji katika sekta ya gesi. Katika mzozo huo, Mengi amemshambulia Waziri Muhongo kwa kumwita ni mwongo, mpotoshaji na mwenye lengo la kuwatoa Watanzania kwenye hoja ya msingi ya rasilimali yao ya gesi. Mengi alitoa kauli hiyo jana kupitia taarifa yake aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari mbalimbali nchini