Siku tatu za maombolezo zaanza nchini Kenya baada ya oparesheni dhidi ya magaidi katika jengo la Westgate kutamatika
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, akiwahutubia wananchi wa Taifa hilo REUTERS/Presidential Strategic Communications Unit Wananchi wa Kenya hii leo wameanza maombolezo ya siku tatu kama ilivyotangazwa na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, maombolezo hayo yanakuja baada ya kutamatika kwa opersehni nzito ya kuwakabili magaidi walioteka jengo la maduka la Westgate toka siku ya jumamosi mwishoni mwa juma lililopita.