Wilshere:Waingereza tu waichezee England
Wilshere huchezea klabu ya Arsenal Mchezaji wa kiungo wa Arsenal na England amezusha mjadala kuhusu matamshi yake kwamba Waingereza tu ndio waiwakilishe timu ya soka ya England. Jack Wilshere alikua akielezea msimamo wake baada ya kijana wa Manchester United Adnan Januzaj kutajwa kwamba anaweza kuichezea England ikiwa atatimiza masharti ya Fifa ya ukaazi wa miaka 5 kwa kua bado hajaamua alichezee taifa gani