Posts

Showing posts from May 22, 2015

MOURINHO NA HAZARD NDIO BORA EPL

Image
Mourinho Mkufunzi wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ametangazwa kuwa mkufunzi bora katika ligi ya Uingereza kwa mara ya tatu. Akihudumia kipindi chake cha pili katika kilabu hiyo rais huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 52 aliiongoza Chelsea kubeba taji lao la kwanza la ligi ya Uingereza katika kipindi cha miaka mitano pamoja na  kombe la Ligi

PENZI LISILOISHA 2

Kijana mdogo, Jafet ambaye alikuwa amehitimu darasa la saba na kufaulu vizuri kuendelea na masomo ya sekondari, anajikuta akikwama kuendelea na masomo kutokana na ufukara wa kupindukia wa wazazi wake. Hali hiyo inamuumiza sana Jafet hasa anapoona wenzake wameanza kwenda shule, muda wote anashinda akiwa analia na kujiinamia kwa huzuni. Mama yake aliyekuwa akijishughulisha na kazi ya kufanya vibarua vya kupalilia mashamba ya mihogo ili apate chakula cha yeye na familia yake, naye anaumizwa sana na hali aliyokuwa nayo mwanaye. Baada ya kumlalamikia na kumlilia sana, mwanamke huyo maskini anaamua kumsaidia mwanaye. Kwa bahati nzuri, anakutana na shoga yake waliyekuwa wakifanya naye vibarua ambaye anamuelekeza kwenda kwenye ofisi za mapadri wa Kijiji cha Rwamgasa, Geita ambako anakutana na padri mzungu, Brocco Giovanni anayeahidi kumsaidia. Anamuagiza kwenda kumleta mtoto huyo ili azungumze naye na kumpa masharti yaliyokuwa yanatakiwa.Je, nini kitafuatia? Usiku huo ulikuw...

PENZI LISILOISHA 1

Karibu kupata stori nzuri imeletwa kwenu na samwelmlawa fwatilia stori hii “ M ama mimi nataka kuendelea na masomo ya sekondari.” “Sasa mwanangu, unajua kabisa sisi wazazi wako hatuna uwezo, wewe unataka kwenda sekondari atakulipia nani ada?” “Ina maana mimi huu ndiyo utakuwa mwisho wangu kielimu wakati nimefaulu? Mbona Alfayo mtoto wa mzee Maguha yeye anaenda sekondari?” “Sasa wale wana mashamba, baba yake kauza shamba moja na ng’ombe ndiyo anamlipia ada, sisi wazazi wako tutauza nini? Hatuna shamba wala mifugo ya aina yoyote, sisi ni maskini mwanangu.” “Mama mimi sikubali, nataka kwenda shule,” kijana mdogo, Japhet Lubongeja alikuwa akizungumza na mama yake lakini walishindwa kufikia muafaka, jambo lililosababisha aanze kuangua kilio na kutoka mbio mpaka nje ya nyumba yao iliyojengwa kwa miti na udongo na kuezekwa kwa nyasi, akakaa chini nyuma ya nyumba hiyo na kujiinamia huku akilia kwa uchungu.