SUALA LA PAPIC, YANGA LASUBIRI UAMUZI WA FIFA!!
Aliyekuwa kocha wa Yanga, Kostadin Papic anaitoa jasho klabu hiyo Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewasilisha rasmi suala la madai ya aliyekuwa Kocha wa Yanga, Kostadin Papic dhidi ya klabu hiyo katika Kamati ya Hadhi ya Wachezaji. FIFA imesema imepeleka rasmi suala hilo katika kamati yake hiyo baada ya kupokea vielelezo vya Papic anayedai kuidai Yanga dola 10,000 za Marekani pamoja na vile vya Yanga inayodai kumlipa kocha huyo fedha zote alizokuwa akiidai klabu hiyo. Kwa taratibu za FIFA, hivi sasa haitapokea vielelezo vingine kutoka pande hizo mbili, na badala yake Kamati hiyo inayoongozwa na Theo Zwanziger kutoka Ujerumani itafanya uamuzi na kuziarifu pande husika. Zwanziger kitaaluma ni mwanasheria. Papic aliyeinoa Yanga kwa vipindi viwili tofauti aliwasilisha malalamiko yake FIFA akidai hadi mkataba wake unamalizika klabu hiyo ilikuwa haijamlipa dola 10,000 za Marekani.