Posts
Showing posts from September 29, 2013
RAIS KIKWETE: ICC INAHARIBU MAHUSIANO YAKE NA AFRIKA
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mwenendo wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kuhusu Bara la Afrika na viongozi wake, unainyima Mahakama hiyo nafasi kubwa ya kuungwa mkono na Bara la Afrika. Rais Kikwete pia amelaani vikali mashambulizi yanayoongezeka dhidi ya vikosi vya kimataifa vya kulinda amani katika nchi mbali mbali duniani wakiwamo walinda amani wa Tanzania.
UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA
- Get link
- X
- Other Apps
HUWEZI hata kidogo kutenganisha maisha ya mwanadamu na elimu ya saikolojia, elimu ambayo katika ulimwengu wa sasa wengi wanaisikia lakini ni wachache wanaotambua umuhimu wake, achilia mbali maana ya neno lenyewe. Injinia wa kwanza aliyeipa nguvu elimu hii ni mwanasaikolojia wa Kijerumani, Wilhelm Wundt ambaye alifungua maabara iliyokuwa ikifanya utafiti na kutibu watu kwa kisaikolojia, zoezi ambalo lilileta matokeo ya kushangaza ulimwenguni. Huo ulikuwa mwaka 1879. Saikolojia ni ‘mtoto’ wa neno la Kigiriki lijulikanalo kama ‘psyche’ au akili na roho jina ambalo baadaye lilikuzwa na kufahamika kama Psychology, tafsiri ikiwa ni Elimu ya Nafsi na Ufahamu. Katika nchi zilizoendelea, somo hili linapewa nafasi ya juu katika maisha ya binadamu kutokana na umuhimu wake. Wanasema wataalamu kuwa, kuishi bila kujua tabia za vitu na watu, ukuaji wake na kujifunza mabadiliko yake ni sawa na kutembea katika kamba ndogo ya maisha salama. http://samwelmlawa.blogspot.com
HATA KAMA UMZURI, BILA UTUNDU FARAGHA HUNA NYIMBO!
- Get link
- X
- Other Apps
Mapenzi yana kanuni zake, kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia. Unapotokea kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa dhati. Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo. Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii wameachika na bado wanaranda mtaani. Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano na mtu na ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa kipekee kwake.