KOCHA KIM PAULSEN WA TAIFA STAR AFUNGUKA NA MECHI YA GAMBIA SEPT 7 2013
Licha ya kupoteza nafasi ya kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia, kocha mkuu wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars Kim Paulsen amesema lengo lake ni kuona kikosi chake kinamaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi C kwa kuifunga Gambia katika mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba utakaochezwa Septemba 7 nchini humo. Stars ambayo ilianza vema michuano hiyo na kuweka hai matumaini ya kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia zitakazochezwa mwakani nchini Brazil kabla ya kupoteza mechi mbili dhidi ya Morroco ugenini na dhidi ya Ivory Coast hapa nyumbani na kujikuta ikiangukia katika nafasi ya tatu kwenye kundi lake linaloongozwa na tembo wa Ivory ccast na kufuatiwa na Morrocco huku Gambia ikikamata mkia. Akizungumza kwenye kambi ya timu hiyo jijini dar es salaam Kim Paulsen amesema baada ya kupoteza nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya kufuzu kombe la dunia sasa amejikita katika kutengeneza kikosi imara kwa ajili ya mashindan...