PLAY GIRL 1 FUATILIA KISA HIKI
"...Jamani mi sijui utaratibu wa hapa., naomba mnirudishie tu huo mkoba wangu.." Nikiwa bado naendelea kulalamika pale uwanja wa ndege, mara akatokea mkaka mmoja mweupe aliyevalia sare za hawa wafanyakazi wa ndege.. "..embu niambie tatizo nini dada mbona unalalamika.." "..Leo ndio mara yangu ya kwanza kupanda ndege na wakati natoka Mwanza hawakunizuia hivi, lakini nashangaa nimefika hapa Dar eti wamezuia mkoba wangu wanadai kuwa hawaruhusu kusafiri na vipodozi kwenye ndege.. Ni haki kweli jamani..?" "..dada unaitwa nani..?"