Watu watano wakamatwa
Meno ya Tembo yaliyokamatwa Zanzibar Polisi nchini Tanzania wamesema shehena ya Pembe za Tembo zilizokamatwa katika bandari ya Zanzibar ni sawa na Tembo mia tatu na watano, zikiwa na thamani ya karibu shilingi bilioni nane, sawa na karibu dola milioni tano za Kimarekani. Watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na pembe hizo, huku maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA, na mmoja wa Mamlaka ya Bandari pia wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.