KAULI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YA IBUA HOJA
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ameunga mkono hatua zinazochukuliwa na Jeshi la Polisi katika baadhi ya maeneo nchini za kuwapiga wananchi. Pinda alitoa kauli hiyo bungeni jana, wakati akijibu swali bungeni akiwataka Polisi kuendelea kutembeza bakora bila woga kwa wananchi wanaokaidi amri zao. Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Mutaza Mangungu, ambaye aliitaka Serikali kuweka wazi kiini cha matatizo ya vurugu badala ya kuwalaumu wanasiasa. Katika swali hilo, Mangungu alisema vyombo vya dola vimeingia katika lawama kwa kudaiwa kuwapiga wananchi bila sababu, huku akitolea mfano wa matukio ya Arusha na Mtwara. Katika majibu yake, Pinda alisema Serikali imechoshwa na vitendo vya vurugu vinavyoendelea nchini, hivyo kwa yeyote atakayekaidi amri ya vyombo vya dola anastahili kupigwa. Pinda alisema, vyombo vya dola havipaswi kulaumiwa na kusisitiza kuwa mtu akiambiwa asifanye hiki akaamua kukaidi, atapigwa tu kwa maana hakuna namna nyingine. Katika kipindi hich...