Mdhalilishaji aliyejidai kuwa Justin Bieber
Mwanamume mmoja nchini katika
kitongoji cha Middlesbrough, Uingereza aliyejidai kuwa mwanamuziki
maarufu duniani , Justin Bieber, ili kuwahadaa watoto kuweza kumtumia
kanda za video wakiwa wanafanya vitendo vya ngono, amehukumiwa kifungo
cha miaka 14 jela.
Robert Hunter, mwenye umri wa miaka 35, na
ambaye alijidai kuwa 'Justin Bieber Hunter 'alikamatwa baada ya msichana
mmoja kutoka Tasmania kufahamisha polisi kumhusu.
Hunter alikubali mashtaka yote 15 yakiwemo kuwachochea watoto kujihusisha na vitendo vya ngono na kutengeza kanda za video zenye picha chafu.
Mahakama ilifahamishwa kuwa kwa miaka mingi Hunter aliwalenga mamia ya wasichana kutoka Uingereza, Ufaransa , Spain, Italy, Serbia, Bara Asia na Canada.
Wasichana walioamini kuwa mwanamume huyo alikuwa kweli Justin Bieber, walijipiga picha wakiwa uchi baada ya Hunter kuwaahidi kuwa angekuwa na uhusiano wa kimapenzi nao.
Lakini walipojaribu kujiondoa kwa mtego wake aliwatumia vitisho.
Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 12, alijikata mikono yake baada ya Hunter kuchapisha picha zake kwenye mtandao akiwa uchi pamoja na anwani yake na nambari zake za simu.
Jaji alisema hii ni kesi mbaya kuwahi kuisikia kuhusu udhalilishaji wa watoto kwenye Internet.
Comments
Post a Comment