YANGA YAKAZIWA NA MBEYA CITY , YALAZIMISHA SARE YA 1-1, MNYAMA ATAFUNA MIWA YA MTIBWA TAIFA, AZAM WAPONEA CHUPUCHUPU KAITABA, JKT RUVU WAZIDI KUPAA KILELENI!!
MZUNGUKO wa tatu wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 umeendelea kushika kasi leo hii kwa timu zote 14 kushuka katika viwanja saba tofauti nchini. Mabingwa watetezi, klabu ya Yanga ya Dar es salaam wameponea chupuchupu mbele ya Wenyeji wa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, klabu ya Mbeya City ambapo wamelazimishwa sare ya 1-1, huku wakishuhudiwa na mwenyekiti wake Yusuf Manji aliyewasili leo mchana. Mbeya City wanaofundishwa na Juma Mwambusi ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 49 kupitia kwa Mwagane Yeyah na Yanga walisawazisha bao hilo katika dakika ya 71 kupitia kwa Mrundi, Didier Kavumbagu “Kavu”. Mbeya City walianza kwa kasi mchezo huo huku wakionana kwa pasi safi na kushambulia lango la Yanga kama Nyuki, lakini makosa ya washambuliaji yaliwanyima mabao ya wazi. Hata hivyo kipindi cha pili Yanga walianza kwa kasi na kushambulia lango la wapinzania wao, lakini dakika za lala salama wakakoshwa bao...