Posts

Showing posts from September 16, 2013

Mdhalilishaji aliyejidai kuwa Justin Bieber

Image
  Rober Hunter aliwahidi watoto kuwa angekuwa na uhusiano wa kimapenzi nao Mwanamume mmoja nchini katika kitongoji cha Middlesbrough, Uingereza aliyejidai kuwa mwanamuziki maarufu duniani , Justin Bieber, ili kuwahadaa watoto kuweza kumtumia kanda za video wakiwa wanafanya vitendo vya ngono, amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela. Robert Hunter, mwenye umri wa miaka 35, na ambaye alijidai kuwa 'Justin Bieber Hunter 'alikamatwa baada ya msichana mmoja kutoka Tasmania kufahamisha polisi kumhusu

RONALDO KUSALIA BERNABERU HADI 2018

Image
Ronaldo anasema Man U ni mambo ya zamani Cristiano Ronaldo amesema kuwa anataka kusalia kuwa Real Madrid kama mchezaji soka baada ya kutia saini mkataba mpya na mabingwa wa ligi ya Uhispania hadi mwaka 2018. Ronaldo ambaye ni mchezaji muhimu wa timu yake ya taifa ya Ureno, awali ilisemekana alikuwa anaelekea Machester United kilabu yake ya zamani....

Ghana kukutana na Misri kutafuta nafasi Brazil

Image
Mashabiki wa soka Ghana wanatumai kuwa nchi yao itafuzu Brazil 2014 Ghana itamenyana na Misri katika mechi za kuamua nchi ya Afrika itakayowakilisha bara zima katika dimba la kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil. Misri kama nchi pakee ambayo imeshinda mechi zake zote za makundi za kufuzu kushiriki kombe la dunia, bila shaka imeitia hofu nchi zengine na bila shaka hakuna ambaye angependa kukukutana nao. Taarifa zinazohusiana...

KESI YA WAZIRI MKUU PINDA YAANZA KUSIKILIZWA SERIKALI YATOA PINGAMIZI KALI

Image
Kesi inayomkabili waziri mkuu Mizengo  Pinda na mwanasheria mkuu wa serikali  imetajwa mahakamnai kwa mara ya  kwanza ambapo  wamewasilisha pingamizi  la  awali dhidi ya  kesi ya kikatiba waliyofunguliwa na kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu  kwa kushirikiana na chama cha wanasheria Tanganyika.    Katika kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2013, LHRC na TLS,wanadai kuwa Pinda alivunja katiba kutokana na kauli  aliyoitoa bungeni hivi karibuni  wakidai kuwa ni amri kwa vyombo vya utekelezaji wa sheria kuwapiga wananchi  wakati wa vurugu.    Hata hivyo Pinda na  mwanasheria mkuu  kwa pamoja katika majibu yao ya madai hayo, wamewasilisha pingamizi la awali ambapo  pamoja na mambo mengine wamedai   kuwa walalamikaji na watu  walioorosheshwa katika kesi hiyo hawana mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo.