Posts

Showing posts from October 29, 2013

Yaya Toure azuru Kenya. Kunani?

Image
Yaya Toure Mchezaji maarufu wa timu ya Manchester City Yaya Toure, amewasili mjini Nairobi Kenya kwa uzinduzi wa muungano mpya wa kukabiliana na uwindaji haramu kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira (UNEP). Muungano huo umeanzishwa ili kukabiliana na uwindaji haramu wa wanyama pori haswa Ndovu ambao wanakabiliwa na tisho la kudidimia kutokana na uwindaji haramu barani Afrika. Toure, mshindi wa tuzo la mchezaji soka bora zaidi Mwafrika kwa miaka miwili mfululizo, 2011 na 2012 ataeleza kwanini amekubali kushirikiana na muungano huo kupambana dhidi ya uwindaji haramu na nini hasa jukumu lake

MBEYA CITY FC YAIBAMIZA TANZANIA PRISONS KWA MAGOLI 2-0

Image
 Mashabiki wa Mbeya City Fc wakishangilia Goli la Kwanza   Mashabiki wa Mbeya City Fc wakishangilia Goli la Pili  Mpira Unaendela ....

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

Image
Unaweza kuzidharau mbegu za maboga, lakini ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, zinazoweza kuzuia na kutibu hata magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi uliokwishafanyika, zifuatazo ni faida za kifya mtu anazoweza kuzipata kwa kula mbegu za maboga, zikiwa mbichi ama zilizokaangwa: HUIMARISHA MOYO, MIFUPA Mbegu za Maboga (Pumkin Seeds), zina kiwango kingi cha madini aina ya Magnesium ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo, uimarishaji mifupa, mishipa ya damu na ufanisi wa utumbo mpana. Magnesium imeonesha uwezo mkubwa wa kuzuia mshituko wa moyo na kiharusi

HAPO ZAMANI ZA KALE: HUKUMU YA WALIOTAKA KUMUUA NYERERE 1983

Image
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Walioshitakiwa kwa uhaini mwaka 1983 walikuwa wengi. Ilielezwa mbele ya jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Nassor Mzavas kwamba washitakiwa walikuwa 19. Miongoni mwao alikuwepo Thomas Lugangira au ‘Uncle Tom’ au ‘Uncle Check bob.’ Wenzake walikuwa ni Hatibu Gandi au ‘Hatty Mac Ghee’, Kapteni Mohammed Tamim, Kapteni Mbogoro,  Kapteni Christopher Kadege,  Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Mapunda. Wengine walikuwa ni Banyikwa na mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Hans Pope , Kapteni Rodrick Rosham Robert  na wengine kibao ambao jumla yao walikuwa 19. Wakati kesi inaendelea Lugangira na Hatty Mc Ghee walipanga njama na kufanikiwa kutoroka kutoka katika Gereza la Keko, Dar.