AKIWA kwenye ziara yake ya kikazi, mara kwa mara Rais Martin alikuwa akipiga simu ikulu kuulizia maendeleo ya mkewe ambaye alimuacha akiwa na hali ya kutatanisha. “Mume wangu, naendelea vizuri ila nina habari njema kwako.” “Ooh afadhali mke wangu kama unaendelea vizuri, unataka kunipa habari gani?” aliuliza Rais Martin huku akionekana kuwa na shauku kubwa. “Wala usishtuke mume wangu kipenzi, mwenzio nime... nime...” alisema First Lady huyo lakini akashindwa kumalizia sentensi yake, akasikika akicheka kwa furaha, jambo lililozidi kumuweka Rais Martin njia panda. “Unaniweka roho juu mke wangu, tafadhali niambie,” alisema Rais Martin huku akionesha dhahiri kuwa na shauku kubwa ndani ya moyo wake, mke wake akamwambia jambo ambalo lilimshtua na kumfurahisha mno