KITUNGUU SWAUMU KINGA YA MAGONJWA MBALIMBALI
Tafiti nyingi zimeshafanyika duniani kuhusu faida za kitunguu swaumu ambazo zimethibitisha kuwa mtu akitafuna na kumeza hata punje moja tu ya kitunguu swaumu kila siku asubuhi, basi mtu huyo atakuwa amejitengenezea kinga ya mwili ya kudumu itakayomlinda na maradhi mbalimbali, yakiwemo maradhi sugu yaliyoshindikana hospitalini. Kitunguu swaumu kimegundulika kuwa rafiki wa damu mwilini, kwani kinapoliwa, huenda moja kwa moja kutoa sumu zote kwenye damu na kuipa damu vitamin na huongeza uwezo wa damu kusafiri vyema katika mishipa hivyo kumfanya mtu ajisikie mwenye afya njema kila siku. Aidha, kitunguu swaumu kimegundulika kuwa na uwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa ya moyo