Familia ya Mandela:'Ni kipindi kigumu'
Wananchi wa Afrika Kusini wamekuwa wakikesha kumkumbuka Mandela Familia ya Hayati Nelson Mandela imezungumza kwa mara ya kwanza tangu Mandela Kufariki Alhamisi. Wameelezea kuwa katika kipindi kigumu huku wakitarajia wiki moja inayokuja kuwa wakati mwingine mgumu kwao. "Msingi wa familia yetu umetuondoka,’’ alisema msemaji wa familia ya Mandela Luteni Generani Themba Matanzima ingawa alisisitiza kuwa Mandela daima atasalia katika mioyo yao.