KURA YA 'HAPANA' YALITIKISA BUNGE LA KATIBA
Dodoma. Wajumbe
wa Bunge la Maalumu la Katiba jana walianza kupiga kura za kuamua ibara
za Katiba inayopendekezwa, huku kura za wajumbe kutoka Zanzibar
zikiibua wasiwasi wa iwapo theluthi mbili itapatikana au la.
Hata hivyo,
mapema Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta alisema idadi ya kura
zinazohitajika kukidhi theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar ni 140 na
jana jioni waliokuwamo bungeni walikuwa 142.
Mjumbe wa
kwanza kufungua pazia kwa kura ya hapana alikuwa ni Adil Mohamed Adil
aliyepiga ibara zote 157 kwa sura ya kwanza hadi 10.
Wengine waliopiga kura ya hapana kwa sura zote ni Dk Alley Soud Nasoro na Salma Said.
Waliopiga kura za hapana ni Fatuma Mohamed Hassan na Jamila Abeid Saleh, huku baadhi ya wajumbe wakipiga kura za siri.
Kwa upande wake, Ali Omary Juma, alikubaliana na sura za 2, 4, 5 na 9 lakini akizikataa sura za 1,3,6,7,8 na 10.
Kwa upande
wa Tanzania Bara, wajumbe Abia Nyabakari na Dk Ave-Maria Semakafu
walipiga kura za ndiyo kwa baadhi ya sura na zingine kuzikataa.
Mjumbe Ali
Keissy Mohamed aliushangaza ukumbi kwa kupiga kura ya ndiyo kwa sura
zote tofauti na wakati akiwa katika vikao vya kamati ambapo alikataa
muundo wa serikali mbili.
Watakaopiga kura kwa faksi
Mwenyekiti
wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta jana alitangaza orodha ya
wajumbe 22 wanaotarajiwa kupiga kura kwa njia ya faksi au mtandao wakiwa
nje ya Bunge hilo.
Katika
orodha hiyo, akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick
Werema, wajumbe tisa wako Saudi Arabia kwa ajili ya Hijja, wawili India
kwa matibabu, mmoja yuko masomoni Uholanzi na wengine nje ya Dodoma
lakini yuko hapa nchini.
Orodha ya wajumbe
Wajumbe
walioko Uarabuni ni Dk Abdalah Kigoda, Mussa Yusuph Kundecha, Hamza
Mustapha Njozi, Mohamed Raza, Dk Maua Daftari, Shawana Bukheri Salum,
Asha Dodo Mtwangi, Amina Andrew Clement na Riziki Lulida.
Wajumbe walioko India kwa matibabu ni Beatrice Shelukindo na Salum Hassan Turk.
Wajumbe
wengine walioko nje ya nchi ni Fredrick Msigala, Waziri wa Afya, Dk Seif
Suleiman Rashid, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela na
Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela.
Comments
Post a Comment