GARDNER ATAKA JIDE AELEZE UKWELI JUU YA NDOA YAO
Stori: Mayasa Mariwata
Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa Bongo ni kitendo cha mtangazaji mwenye jina kubwa wa Kipindi cha Maskani cha Redio Times FM, Gardner G Habash ‘Kepteini’ kutaka mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ndiye aeleze ukweli juu ya ndoa yao
.
Akizungumza kwenye Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani kupitia Televisheni ya EATV chini ya ‘hosti’ wake, Salama Jabir, Jumanne iliyopita, Gardner alikataa kuzungumzia ndoa yake inayodaiwa kuvunjika.
Pamoja na mambo mengine ambayo aliyajibu kwa ufasaha, Gardner alipoulizwa juu ya habari zinazozungumzwa mtaani kuhusu kuvunjika uhusiano wake na Jide au Lady Jaydee, aligoma kulizungumzia kwa kigezo kwamba kipindi hicho kilimhusu yeye tu.
Mtangazaji huyo alikwenda mbele zaidi kwa kumwambia Salama kwamba amwite Jaydee kwenye kipindi hicho ili alielezee jambo hilo kwa undani.Gardner na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa wakidaiwa kuwa hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki huyo yakielea.
Kupitia kipindi chake cha Diary of Lady Jaydee kilichokuwa kikisimamiwa na Gardner ambacho sasa kinaongozwa na ndugu wa msanii huyo aitwaye Wakazi, Jumapili iliyopita Jide alionekana kwenye harusi ya ndugu yake aitwaye Lameck Mbibo ‘Dabo’ ambaye pia ni msanii wa Dance Hall akiwa mpweke bila mumewe kama ilivyozoeleka.

Comments
Post a Comment