DOKTA MIMI SIUMWI HUKO (sehemu ya kwaza fwatilia kisa hiki chakusisimua)

Ulikwenda hospitali mke wangu?” Masofa alimuuliza mke wake Sulee.
“Nilikwenda, lakini daktari kasema mimba nitapata tu ndani ya mwezi mmoja.”
“Ndani ya mwezi mmoja utapata mimba? Inawezekana kweli? Hujamwambia kwamba tumehangaika kutafuta mtoto kwa miaka nane, sasa ndani ya mwezi mmoja mimba itapatikana vipi?”
“Mimi sijui Masofa.”
“Mh! Haya, kwa sababu tumeambiwa na mtu tunayemwamini tuangalie, labda kweli daktari yule atatusaidia. Hakusema uende na mimi?”
“Hakusema Masofa, ila alisema kama naweza kesho na keshokutwa niende usiku saa moja ili anipime vizuri.”
“Alikupa
dawa?”
“Dawa atanipa kesho.”
Masofa alichukua simu akampigia rafiki yake Miraji...
“Ee bwana Miraji, yule dokta uliyemsema kasema ‘waifu’ aende kesho saa moja usiku, wewe si unamwamini?”
“Yule hana neno, aende tu. Bwana Masofa we hukumbuki jinsi mimi na shemeji yako tulivyohangaika kutafita mtoto?”
“Nakumbuka.”
“Sasa kama si huyo daktari wa wanawake unadhani tungepata mtoto?”
“Oke, nimekuelewa bwana Miraji.”
“Sawa Masofa.”
Masofa alikata simu, akaendelea kukaa chumbani. Akili yake ilikuwa nzito sana kumruhusu mkewe arudi hospitali kesho yake, tena usiku wa saa moja...
“Sasa huyo daktari wa watoto ni kwa nini anataka mke wangu arudi usiku? Ni tiba gani hiyo ya usiku wa saa moja?”
***
Siku ya pili iliingia, saa moja jioni Sulee alikuwa kwa daktari wa wanawake anaitwa Dokta Kisarawe.
Dokta Kisarawe alikuwa amekaa ndani ya chumba cha utabibu kwenye zahanati yake huku akimwangalia Sulee kwa macho yenye huruma...
“Kwa hiyo tatizo kubwa ni mtoto tu anti yangu?”
“Ni mtoto tu.”
“Miraji unamjua?”
“Ndiyo, ni rafiki wa mume wangu Masofa kwani vipi dokta, mbona umemtaja huyo?”
Usikose kusoma wiki ijayo kwenye blog yasamwelmlawa.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU