NINI MAANA YA MAPENZI
MAPENZI
Kila binadamu
hupenda jambo fulani. Mapenzi ya mtu juu ya jambo yaweza kumvutia kiasi kwamba
anaweza kupoteza welekeo wa maisha yake. Watu hupenda hadi kileleni. Hapa ndipo
mtu aelewi hili wala lile. Hali hii si tu kwa vijana wanaoingia katika umri wa
balehe bali hata kwa wale waliovuka umri huu. Kweli kila mtu anahaki ya
kupenda. Na mapenzi haya yalianza pale binadamu walipoanza kuishi pamoja kama
mke na mume kama vitabu vyetu vya dini
vinavyoelekeza, ambavyo ni Biblia na Kuruhani.
Napenda kuwa
muwazi sana juu
ya aina ya penzi ninalozungumzia. Ni yale mahusiano ya kimwili yaliyopo kati
mwanamke na mwanaume. Haya ndiyo mahusiano ninayozungumzia na sizungumzii yale
ya watu wa jinsia moja. Mapenzi hayauzwi na ayachagui rangi wala kabila.Mapenzi
ni kitu asilia ambacho humkuta mtu juu
ya mtu mwingine ambaye anaweza kuwa mwanamke kwa mwanaume au kinyume chake. Na
hawa kila mmoja hutokea kumpenda mwenzake mpaka kufikia kilele cha penzi.
Angalia mfano
huu; umepita wapi na kutembea mikoa mbalimbali au wilaya, tarafa, kata, vijiji
na mitaa mingapi? Umekutana na wangapi wazuri (wanawake au wanaume), na
ulimpenda yupi. Inawezekana kati ya uliowachagua hakuna hata mmoja kati ya wale
uliokutana nao ukaridhia kuwa naye. Lakini ulikutana na kijana mmoja ambaye
amekuvutia sana
zaidi ya asana na mahusiano ukaanza kuanzisha mpaka leo ni mke wako au mchumba
wako. Hapo ndipo ninaposema “love is something natural” na si
kitu cha kubahatisha tu.
Na ieleweke kwamba mke mzuri ni wako tu, na
mme mzuri ni wako tu. Hakuna ubishi kwa hili. Na pale unapoona kuwa mke au
mme wako si mzuri basi ulikosea wakati wa uchaguzi wako. Hapo huna budi kuonyesha unampenda kama kitabu hiki kinavyoeleza uk.6 & 7. Na ujue
kwamba kila mtu ana haki ya kupendwa na mme, mke au mchumba wake. Penye upendo pana mapenzi ya kweli.
NINI MAANA YA MAPENZI?
Neno mapenzi ni pana sana. Na kila mtu huweza kufikiri kulingana
na uelewa wake juu ya mapenzi kati ya mtu na mtu. Mapenzi ni ile hali asilia
ambayo mtu anakuwanayo kwa mtu mwingine na inapaswa kuwa na makubaliano baina
ya wahusika ambayo yaweza kuwa ya muda mfupi au muda mrefu. Wengine husema
mapenzi ni ile hali ya mtu kuwa na mahusiano ya kimwili na mwingine.
Kipindi
tulichopo sasa ni kipindi cha utandawazi.
Si mtoto mdogo si wakubwa wote wanayafahamu mapenzi yalivyo. Kwa sasa imekuwa
kawaida kwa kila mtu kuanza uhusiano hata kabla ya kufunga ndoa. Hii ndiyo
ninayoita utandawazi. Watoto wadogo hupata habari hizi kupitia masimulizi
kutoka kwa kaka na dada zao nyumbani au nje. Hii haikuwa tamaduni yetu, lakini
sasa ni jambo la kawaida kwa mwanafunzi wa darasa la tano kukutwa na ujauzito.
Lakini ni kwa mazingira hayahaya.
Kipindi hiki
ndicho kipindi kigumu kwa vijana kujua yupi ni mke/mme mwema na yupi si mke/mme
mwema. Athari hizi huwakuta sana
akina dada ambao wakizidisha miaka ishirini na saba, yule ambaye alikuwa mme
mzuri anampoteza ndani ya miaka 18 hadi miaka ishirini. Ndani ya miaka hii
mwanamke huvutia na anaonekana kama ua
linalovutia wadudu (Dr Isack Ndodi, 2011). Nakubaliana sana na maneno ya Dr. Ndodi akizunguma Channel 5 kati ya mwezi Mai hadi Juni,
2011.
Kuna ukweli
uliopo juu ya hili. Ndani ya miaka hii mwanamke ujikuta anaingia katika
majaribu yasiyo na msingi huku akijitahidi kutafuta mme mzuri kwake, na matokeo
yake huishia kuchezewa na hatimae kukosa wote. Wanaume ndio wasababishaji
wakubwa wa mke huyu asiolewe au asipendwe. Angalia mfano huu, mti ukichipuza maua utamuona mdudu wa
kila aina akiwemo nyuki, nzi, kipepeo na wengine wemgi wakiingia na kutoka.
Haya ndiyo yaliyopo kwa wanawake kwa kipindi hicho tajwa hapo juu.
Hapa lile neno
langu love is something natural (mapenzi ni kitu cha asili) hutumiwa vibaya na
badala yake mapenzi hupoteza umaana wake. Kwa kila mtu mwenye upendo wa kweli
hawezi kumdarau mchumba au mke/mme wake. Na inapotokea vinginevyo ni makosa ya
kibinadamu ambayo hutokea baina ya hawa wapendanao.
Comments
Post a Comment