UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA

HUWEZI hata kidogo kutenganisha maisha ya mwanadamu na elimu ya saikolojia, elimu ambayo katika ulimwengu wa sasa wengi wanaisikia lakini ni wachache wanaotambua umuhimu wake, achilia mbali maana ya neno lenyewe.
Injinia wa kwanza aliyeipa nguvu elimu hii ni mwanasaikolojia wa Kijerumani, Wilhelm Wundt ambaye alifungua maabara iliyokuwa ikifanya utafiti na kutibu watu kwa kisaikolojia, zoezi ambalo lilileta matokeo ya kushangaza ulimwenguni. Huo ulikuwa mwaka 1879.
Saikolojia ni ‘mtoto’ wa neno la Kigiriki lijulikanalo kama ‘psyche’ au akili na roho jina ambalo baadaye lilikuzwa na kufahamika kama Psychology, tafsiri ikiwa ni Elimu ya Nafsi na Ufahamu.
Katika nchi zilizoendelea, somo hili linapewa nafasi ya juu katika maisha ya binadamu kutokana na umuhimu wake. Wanasema wataalamu kuwa, kuishi bila kujua tabia za vitu na watu, ukuaji wake na kujifunza mabadiliko yake ni sawa na kutembea katika kamba ndogo ya maisha salama.http://samwelmlawa.blogspot.com

Saikolojia ni somo ambalo kila kukicha binadamu anatakiwa kufundishwa kwa vile hakuna anachoweza kukifanya kisiguse akili na nafsi yake. Inashauriwa kwamba ni lazima mtu ajifahamu mwenyewe, awafahamu wengine, mazingira anayoishi na mabadiliko yake.
Maswali ya msingi yenye kumuongoza binadamu vizuri katika maisha yake ni haya; Mimi ni nani, kwa nini niko hivi? Wale ni 80 akina nani, kwa nini wako vile na tunapaswa kuwa vipi baadaye, pamoja na kujiuliza kwa nini vitu vipo kama vilivyo.
Imebainika kwamba, mvutano wa nguvu za dunia na za binadamu huongezeka mara dufu kwa mtu ambaye hajui Saikolojia ya Maisha. Dunia kama sayari na mwanadamu kama kiumbe kila mmoja amekuwa akitengeneza nguvu zake za kumuwezesha kuwepo, huku uzalishaji wa nguvu hizo kwa upande mmoja ukikinzana vikali na mwingine, hata hivyo madhara makubwa yamekuwa yakiwakuta binadamu ambao ndani yao kuna uhai.
Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kwamba, ufahamu wa nafsi na akili umebaki kuwa kinga muhimu ya mwanadamu katika ulimwengu huu ambao umekuwa ukibadilika mara kwa mara.
Hatari inayokuwepo kwa baadhi ya binadamu siku hizi hasa wa ulimwengu wa tatu, ni ukosefu wa elimu hii muhimu, jambo ambalo limewafanya watu wenyewe kwa wenyewe kuzalishiana nguvu za kuangamizana na kuiacha dunia ikishinda.
Inahuzunisha pia kufahamu kwamba, mbali na binadamu kushindana na mabadiliko ya ulimwengu na nguvu zake, wengi wao wamekuwa wakipambana na nguvu zao wenyewe ndani ya miili yao bila kujijua, kiasi cha kupoteza maisha.
Tafiti za wanasaikolojia zinaonesha kwamba, asilimia kubwa ya matatizo yanayomwangaisha binadamu yanatokana na yeye mwenyewe au jamaa zake, huku ushahidi ukionesha kuwa hata magonjwa ya kutisha kama ya moyo, kansa, kisukari, vidonda ya tumbo na mengineyo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na mawazo ya watu wenyewe.
Itaendelea wiki ijayo.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU