Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu yabariki Saudi Arabia kukataa uanachama katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Saud al-Faisal katika moja ya mkutano
Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Saud al-Faisal katika moja ya mkutano
Reuters/路透社

Jumuiya ya nchi za kiarabu imeunga mkono hatua ya Saudi Arabia kutupilia mbali nafasi ya uanachama wa muda iliyopewa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa madai kuwa baraza hilo limeshindwa kusuluhisha mizozo katika nchi za kiarabu.

Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo Nabil al-Arabi amesema Saudi Arabia ilikuwa na haki ya kutupilia mbali kiti hicho kutokana na baraza hilo kushindwa kurejesha amani katika nchi mbalimbali ulimwenguni.
Nabil amesema mataifa ya nchi za kiarabu hususani Palestina na Syria yametaabika sana katika kipindi hiki kutokana na udhaifu wa baraza hilo.
Wanadiplomasia wengi wanaona hatua ya Saudi Arabia kukataa nafasi hiyo ni ujumbe tosha kwa Marekani kuwa hawaridhishwi na jinsi wanavyojihusisha na mgogoro wa Syria na kuwa imekasirishwa na hatua ya Washington kujihusisha na Tehran.
Hata hivyo kuhusu mzozo wa Syria Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika nchi za kiarabu Lakhdar Brahimi amesema kuwa hakuna tarehe iliyotengwa kuanza kwa mazungumzo ya amani kuhusu Syria.
Kauli ya Brahimi inakuja kutokana na wapinzani kutofikia maamuzi ya mwisho na kuamua iwapo watashiriki katika mazungumzo hayo ambayo yalipangwa kufanyika mwezi Novemba.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

NINI MAANA YA MAPENZI