DRC yasitisha mazungumzo na M23
Mazungumzo ya amani kati ya
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23 yamesitishwa
tena licha ya Umoja wa Mataifa kuweka msukumo wa kuendelea kwa
majadiliano ya pande hizo mbili.
Mazungumzo hayo yamekuwa yakiendelea mjini
Kampala Uganda tangu Septemba mwaka huu ambapo kila upande umetoa tamko
lake kuhusiana na kusitishwa kwa mazungumzo hayo.
Msemaji wa Serikali ya Kongo Lambert Mende amesema kuwa mazungumzo yamesitishwa kutokana na kutofikiwa makubaliano kuhusu msamaha kwa M23 na jinsi watakavyo jumuishwa katika jeshi la Taifa la nchi hiyo FARDC.
Mjumbe wa M23 katika mazungumzo hayo Roger Lumbala alisema kumekuwa na vikwazo lakini wao wako tayari kurejea kwenye meza ya majadiliano wakati wowote.
Awali serikali ilionya kuwa majadiliano yaliyoanza upya mwezi Septemba chini ya shinikizo la Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu yalikuwa yanakwenda taratibu mno hali iliyoashiria mwisho wa maafikiano.
Comments
Post a Comment