Dakar kumzika Kocha wa zamani Bruno Metsu

Bruno Metsu kuagwa na kuzikwa nchini Senegal
Bruno Metsu kuagwa na kuzikwa nchini Senegal

Raia nchini Senegali mjini Dakar wanatarajia kuhudhuria mazishi ya Kocha Mfaransa Bruno Metsu ambaye aliaga dunia juma lililopita baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani.

Mfaransa huyo ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 59 alichangia sana kuifikisha timu ya Senegali hatua ya robo fainali ya michuano ya kuwania kombe la dunia 2002 michuano iliyofanyika nchini Japan.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirikisho la soka barani ulaya kupitia mtandao wake,kocha huyo amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani na mauti yalimfika akiwa Ufaransa
.
Bruno ametumikia timu mbalimbali barani ulaya kwa takribani muongo mmoja kabla ya kuja barani Afrika 2000 ambako alipewa jina maarufu la White Sorcerer.
Alikiongoza kikosi cha Senegali enzi hizo kilipojuliana kama simba wa Teranga, akiwa na mvuto na mbinu zenye ushawishi mkubwa.
Kikosi cha Senegal kilishangaza wengi ndani na nje ya bara la Afrika kwa kuishinda Nigeria na kufikia hatua ya fainali ya kombe l amataifa ya Afrika mwaka 2002 ambapo ilipoteza baada ya kushindwa na Cameroon.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU