Atuzwa kwa kutetea elimu kwa wasichana


Malala alipigwa risasi kichwani kwa kutetea haki za wasichana kusoma
Msichana mwenye uraia wa Pakistan ambaye pia ni mwanaharakati wa elimu , Malala Yousafzai, aliyepigwa risasi kichwani na wapiganaji wa Taliban, ameshinda tuzo la wanaharakati wa haki za binadamu la Sakharov ambalo hutolewa na Muungano wa Ulaya.
Malala mwenye umri wa miaka 16 alipigwa risasi mwaka jana kwa kutetea haki za wasichana kupata elimu.

Tuzo la Sakharov hutolewa na bunle la ulaya kila mwaka kwa heshima ya mwanafisikia wa kisovieti Andrei Sakharov.
Mwengine ambaye alioneka kuweza kuipata tuzo huyi ni Mmarekani Edward Snowden aliyefichua siri ya Marekani kudukua taarifa za faragha za watu.
Tuzo hiyo ni ya thamani ya dola (65,000) .
Malala alianza kusifika duniani mwaka 2009 baada ya kuandika blogu kuhusu maisha yake chini ya utawala wa Taliban kwa niaba ya idhaa ya Urdhu ya BBC,na kuelezea changamoto ya wasichana kupata elimu nchini humo.
Alikuwa anaishi katika eneo la bonde la SWAT na jina lake lilikuja kujulikana baada ya jeshi kufurusha wapiganaji kutoka eneo hilo mwaka 2009.
Kundi la Taliban huwawekea vikwazo sana wanawake na kukandamiza haki zao na mmoja wa wapiganaji hao alimpiga risasi alipokuwa ndani ya basi kuelekea nyumbani.
"leo tungependa kueleza dunia kuwa matumaini yetu yako mikononi mwa vijana kama Malala Yousafzai, '' alisema kiongozi cha chama cha Ulaya cha conservative Joseph Daul.
Malala alishangiliwa sana kwenye mkutano wa baraza la umoja wa mataifa alipotoa hotuba kusema kuwa kamwe hatanyamazishwa.
Watu wengine ambao wamewahi kupokea tuzo hiyo ni pamoja na Nelson Mandela wa Afrika Kusini na Aung San Suu Kyi ambaye ni kiongozi wa upinzani Burma.

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU