NORA NA WATEMANA GEOFREY


UHUSIANO wa wasanii wawili wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ na Geofrey Kusila umeota mbawa baada ya kumwagana na kila mmoja kuendelea na maisha yake.

Nuru Nassoro ‘Nora’.
Chanzo makini kilicho karibu na wasanii hao kimepenyeza habari kuwa uhusiano wao umevunjika bila kufahamika chanzo.
“Nora na Geofrey wameshaachana na kila mtu ana maisha yake hata kazi hawafanyi tena pamoja, tangu walipoachana Nora anaandaa kipindi chake cha kwenye runinga na hayupo tena na Geofrey,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Nora ili kuujua ukweli, akafunguka:
“Mimi ninafanya kazi zangu mwenyewe na Geofrey kivyake kwa sababu tumeachana na kampuni ambayo tulikuwa ndiyo kwanza tumeianzisha nayo imekufa na baada ya hapo kila mmoja akashika njia yake na kuangalia jinsi gani atakavyofanya kazi hivyo hatupo pamoja tena.”

Comments

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

NINI MAANA YA MAPENZI

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU