SIFA ZA MABANDA YA KUFUGIA KUKU

Banda la kuku

Katika ufugaji wa kuku itakiwa kuwa na ubunifu wa banda la ufugiaji kuku ili kuboresha uzalishaji wa kuku bora wenye afya nzuri na wasiweze kushambuliwa na magonjwa mbalimbali kwa mazingira ya mabanda yakiwa ayana ubora ni  tatizo.

Kuna watu wameweka fikra za ufugaji lakini awazii banda la kuwaweka kuku linatakiwa likizi vitu gan ili aweze kufuga.
       SIFA ZA BANDA ZURI LA KUKU:   
  1. kuwe na hewa yakutosha kwenye ilo banda.
  2. kuwe na mwanga wakutosha
  3. liwe na uwezo wakupitisha mionzi ya jua(miyale ya jua)inayo chomoza maghalibi ya banda lako na mashariki ya banda
  4. lenye ukubwa mzuri ambao inategemea na kuku unaotaka kufuga
  5. n.k



Hewa ni muhimu kwa kila kiumbe, hivyo banda la kuku ni lazima liingize hewa safi na kutoa ile chafu na liweze kuingiza mwanga wa kutosha.
1. Kwa kifupi ni kwamba madirisha ya banda ni lazima yawe makubwa na ya kutosha ili yaingize hewa safi na kutoa ile chafu.
2. Ni vema madirisha haya yawe juu kiasi cha meta moja (1) kutoka chini ili hewa ipite juu ya vichwa vya kuku.
3. Hewa safi siyo upepo, hivyo jaribu kuzuia upepo mkali kuingia ndani ya banda la kuku ama sivyo kuku wataugua ugonjwa wa mafua na niumonia na vifaranga vinaweza kufa kwa ugonjwa wa baridi.
4. Jenga Banda lako kwa kukinga upepo unakotokea na kupanda miti kuzunguka banda hilo la kuku ili kupunguza kasi ya upepo na kuweka kivuli dhidi ya jua kali na joto.
UKAVU NA USAFI WA NDANI:
Kwa vile kuku si ndege wa majini kama bata , ni jambo la busara kuhakikisha kuwa mahali anapoishi hapana unyevunyevu.
1.       Banda la kuku lijengwe mahali palipoinuka ili kuzuia maji ya mvua yasiingie.
2. Wajengee kuku uchaga wa kulalia kwa kuweka viguzo vyenye urefu wa meta moja na kutandika miti juu yake ili usiku walale hapo, kuliko kuwalaza ardhini au sakafuni.
3. Ukavu wa banda ni muhimu sana hasa kwa vifaranga na kuku wanaotaga. Ndani ya banda lenye unyevu mayai kuchafuka sana hata wakati mwingine huoza kwa urahisi na jitihada zako zitakuwa ni bure.
4. Sakafu ya banda ni vizuri ikawa ya zege lakini kutokana na uhaba wa fedha sakafu inaweza kutengenezwa kwa mabanzi (mabanda yaliyoinuliwa) au udongo mgumu na au mchanga ambao utafunikwa kwa mabaki ya taka za mpunga na yale ya mbao.
5. Ili kuepuka unyevunyevu ni vyema eneo/mahali pla kujenga banda pawe pameinuka na penye kupitisha hewa ya kutosha.

PAA LA BANDA:
Paa la banda liwe madhubuti ili kuzuia maji ya mvua kuingia hasa wakati wa masika. Sakafu ya banda iwe juu zaidi ya usawa wa nje. Paa linaweza kuezekwa kwa mabaki ya vipande vya bati , madebe na kama ikishindikana tumia nyasi zinazofaa kwa ajili ya kuezeka nyumba katika eneo hilo.

MATANDIKO
Nilazima kuweka matandio katika sakafu ya banda la kuku. Sehemu ambayo kukuwakubwa wanaweza kutagia. Ni vizuri kutumia maranda, na si Pumba zinazo tokana na mbao
Kuku wanaweza kula pumba za mbao. Kwa kuku wanaohatamia, vipande vidogo na vilaini vya miti na makapi kama vile pumba za mpunga zinaweza kutumika

NAFASI YA KUFANYA KAZI:
Banda la kuku lisiwe na nguzo au mbao nyingi sana ndani kiasi cha kumfanya mhudumiaji wa kuku ashindwe kufanya kazi zake. Hali hiyo itamfanya apoteze muda mwingi katika kuzizunguka nguzo hizo, hasa wakati wa kuokota mayai au kufanya usafi.

VIFAA:
Unapotaka kujenga banda la kuku kwanza kabisa tayarisha vifaa vinavyotakiwa. Vitu kama miti au nyasi, nyavu au fito, misumari au kamba ni muhimu kuviandaa mapema.
Pili ni lazima uwe na plani/ramani kamili ya banda hilo. Kwa wastani kila kuku anahitaji nafasi ya Meta za eneo la 0.11 hadi 0.22 (futi 1 hadi 2 za eneo.) kutegemeana na umri wa kuku.

UJENZI RAHISI:
Kuku wafugwao hatimaye ni lazima wafidie gharama za Ujenzi wa mabanda na chakula. Gharama zikiwa kubwa sana huenda ukaifanya shughuli ya ufugaji isiwe na faida hata kidogo hali hiyo itamfanya mfugaji aone ufugaji hauna maana yoyote kwake. Lakini ukijenga banda lako kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi utaongeza faida zaidi kwakuwa umepunguza gharama za uendeshaji wa mradi.

VIPIMO:
Banda la kuku linatakiwa liwe na Meta 15 hadi meta 22 za eneo yaani Meta 3 hadi 4.5 za upana kwa meta 5 za urefu. Banda hili linaweza kutunza kuku 100 wakubwa kwa wakati mmoja.
HITIMISHO:
• Ujenzi wa mabanda unasisitizwa katika kuboresha ufugaji wa kuku wa asili ili;
• Kuongeza uzalishaji na kupunguza vifo vya vifaranga kwa majanga mbalimbali kama vicheche, mwewe, mapaka, mbwa na wizi wa kuku wanaozurura holela.
• Vile vile inatarajiwa kwamba kuku wanaozuiliwa kwenye banda na kuwekewa chakula mchanganyiko wataongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.

MIFANO YA MABANDA BORA
Hii ni mifano ya mabanda bora ya kuku yanayotengenezwa Tanzania na yanafaa zaidi kwa wafugaji wenye maeneo ya mijini ambako maeneo ya ufugaji ni shida zaidi.

Hii ni mifano ya mabanda yanaweza kutengenezwa ili kboresha ufugaji wa kuku











Comments

  1. safi, na nimevutiwa na Maelezo mazuri kabisa... je naweza kumpata fundi mzuri atakaye weza kunijengea banda zuri na la kisasa? namba zangu ni 0713-453532

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

TUMIA SMS HIZI KUBORESHA PENZI LENU

FAIDA TISA ZA MBEGU ZA MABOGA KATIKA MWILI WA BINADAMU

UMUHIMU WA KUJIFUNZA SAIKOLOJIA